''BEN POL'' BONGO FLAVA MUSIC ARTIST ASOKUWA NA SKENDO!!!!!! BANJUKA WITH HIS BIOGRAPHY HAPO CHINI....

Basic Information

Genre
RnB & Soul
Hometown
Dar Es Salaam
Record Label
: M LAB
Ni msanii anayekuja kwa kasi na ni mmoja wa vijana aliye chini ya usimamizi wa Duke Tachez kutoka M lab studio ambayo iko chini ya Duke. Jina lake Halisi ni Benard Paul mtoto wa pili katika familia ya watoto wanne, lakini kwa jina la kisanii anajulikana zaidi kama Ben Pol.
Ben Pol alianza kujigundua kuwa ana kipaji cha muziki akiwa Darasa la Tano ambapo nyimbo yake ya kwanza aliandikiwa na Baba ya...ke mdogo hiyo ilikua mwaka 2001. na akaachana na mambo ya muziki na kufanya sanaa za shule zaidi ikiwa na kuigiza na mambo mengine.Kufikia Form two Ben Pol alikutana na Msanii mwenzake ambaye kwa sasa wako label moja anayejulikana kama Stereo. Hii ilitokana na kuwa msiri kwa mambo yake. Na kwa mara ya kwanza aliandika Verse yake mwenyewe na stereo kugundua kuwa ana style nzuri ambayo ingeweza kumuweka juu kimuziki na stereo kumtambulisha kwenye studio ya kaka yake iliyokua ikiitwa Big Boys producer akiwa ni Prof Ludigo.

Siku ya kwanza kuingia studio hapo hawakufanikiwa kurecord kwa sababu ya umeme kukatika. Wakiwa kwenye harakati ya kutafuta kutoka kimuziki, Waliingia kwenye Tamasha la WAPI na walifanikiwa kukutana na watu kama Joh Makini, Fid Q na wengine kibao. na mtu aliyemshawishi zaidi ukiacha stereo, Ni kama Prof Jay ambaye kwa kipindi iko na mpaka sasa ni mtu ambaye alikua akwepeki kukufanya uwe unampenda na Ben Pol kutamani kuwa mwanamuziki. Kufikia Form 4 mwaka 2006 – 2007 alifanikiwa kutoa nyimbo ambayo ilikua inaitwa nikupendae ambayo ilikua na Mistari minne tu. ambayo ilikua ijijirudia na baada ya kumuonesha stereo alimshauri kuanza kuimba na si kurap. Na stereo alipata wazo la kumshauri kuacha kurap na aanze kuimba kama wasanii wengine kama Barnaba, Amini na wengineo.


Ben Pol hakuweza kujikita zaidi kwenye zaidi kwenye muziki kwa kipindi icho kutokana na shule na kuona wakati utafika na atakuja kuanza kufanya Rasmi. Mwaka 2009 Ben Pol kwa mara ya kwanza aliitwa Mlab kuingiza Hard Lips kwenye wimbo wa Musa vipaji vingi ambao wimbo huo Ben pol alishiriki kuandika maneno ya Kigogo.
Baada ya kumaliza ya kumaliza Shule 2010, Ben Pol alifanikiwa kuingia mkataba na M lab hii ilitokana baada ya producer Duke kujua kipaji cha Ben Pol na kuona wanaweza kufanya pamoja na Siku ambayo Duke alimkubali zaidi Ben Pol siku ambayo Nikki Mbishi alikua akifanya track yake ya Play Boy na Ben Pol alipita Studio kusalimia na bahati nzuri alifanikiwa na kuombwa kufanya Part ya kiitikio cha Play Boy. Kiukweli Ben Pol alifanya vizuri katika kiitikio hicho na kuzidi kumshawishi Duke kumuhitaji zaidi kufanya nae kazi. na Duke alimuhita kwa mara ya mwisho na kumfanyia majaribio ya mwisho ambayo alipewa beat ambayo aliyotakiwa kuandikia na Ben Pol kwa mara ya kwanza alifanikiwa
kurecord track yake iliyokwenda kwa jina la PATA RAHA
ambayo aliandika akiwa studio na alifanikiwa kuwashirikisha wasanii wenzake ambao ni Stereo, One na nikki mbishi.
Ben Pol safari yake ya kimuziki ikaanzia hapo na wimbo kuanza kupigwa katika vituo mbali mbali vya Radio na Ben Pol akaingia mkataba rasmi na M lab wa kufanya kazi zake za kimuziki. na kufanikiwa Kurecord nyimbo ya pili ambayo ilikwenda kwa jina la NIKIKUPATA amabayo iko Radio na inazidiki kufanya Vizuri
Ben Pol akuishia Hapo ameshawahi shirikishwa katika nyimbo kadhaa kama Play Boy ya Nikki Mbishi na My Time ambayo amehirikishwa na Nendeze, Angeris, baby Jay, Pipi, Linah, Mary Lucas, Aneth, Chiku K & Vanessa. hii ni Nyimbo ambayo imetoka Hivi karibuni ikiwa imefanywa M lab na Producer Duke ambaye anafanya Mixtape ya New Era Muzik. SIKILIZA HAPA.
Ben Pol kwa sasa yuko mbioni kutoa video yake ya nikikupata ambayo amefanya na Adam Juma wa visual Lab ambayo itatoka hivi karibu. na yuko mbioni kutoa album ambayo bado hajaipa jina na iko jikoni na soon itatangazwa jina.
Ben Pol anatoa shukrani kwa Wazazi wake kwa kumpa moyo, mashabiki wake kwa kumsapoti katika shughuli zake za kimuziki na kupokea kazi zake vizuri, Producer Mbezi, THT, Musa Vipaji Vingi, Stereo, na management nzima ya Mlab na wengine Wengi ambao kwa namna yoyote wamefanikiwa kumsaidia katika shuguli zake za kimuziki.
 

Huyo Ndo Ben Pol wadau

Press Contact
+255 225504222

No comments: