MUENDELEZO WA PICHA NYUMBANI KWA MAREHEMU ''STEVEN KANUMBA a.k.a KANUMBA THE GREAT''' SINZA,VATCAN-JIJINI DAR ES SALAAM

 Mkurugenzi wa Global Publisher, Erick Shigongo

H-BABA akihojiwa na waandishi wa habari
Wadau na mashabiki wa marehemu
Mwigizaji Mainda (second left) with Breach akimfariji shost wake
 With Super Model Millen Magese nyumbani kwa marehemu Kanumba
  Shigongo wa Global Publisher akifanyiwa interview
Ruge wa Clouds FM alisema, ni pengo kubwa sana kwani katika sanaa alikuwa anahitajika sana
Steven Charles Kanumba alizaliwa januari 8, 1984, akiwa ni Msukuma kutoka mkoani Shinyanga alipata elimu yake ya Msingi katika shule ya Msingi Bugoyi mkoani humo. 
Alipo maliza elimu yake ya Msingi Kanumba alijiunga na elimu ya Sekondari katika shule ya Mwadui seminari na baade alipofika kidato cha pili kuhamia katika Shule ya Christian a Seminari iliyopo jijini Dar es Salaam. Alihitimu kidato cha sita katika shule ya Sekondari Jitegemee inayomilikiwa na Jeshi .
Kanumba amefariki huku akiwa anamfikiria msanii mwenzake Kajala Massanja ambaye yupo Segerea, kwani ndiyo Posti yake ya mwisho alotuma kwenye mtando wa kijamii Facebook. Akilalamika kuhusu roho mbaya walonayo wasanii kwani Kajala yupo Segerea lakini hakuna mtu yeyote katika tasnia ya filamu nchini inayomsapoti msanii huyo. 
Kanumba atakumbukwa kwa mengi sana, Katika historia ya tasnia ya filamu nchini Tanzania, Kanumba ndiye aliyekuwa msanii wa kwanza nchini kufanya kazi nje ya nchi na kuweza kuwavuta wageni kutoka nchi mbalimbali kuja kuigiza Tanzania. Hasa walikuwa Wanigeria kama vile Mercy Johnson, Emmanuel France, Nkiru Silvanus, Ramsey Nouah, na wengine wengi tu. Kanumba pia ameweza kuwaleta waongozaji filamu kadhaa was Kinigeria nchini.
Kanumba alipata mwaliko wa kushiriki katika tamasha kubnwa la Filamu la Nchini Ghana ambalo linajulikana kamam Festival of Films in Africa (FOFA 2012) lililofanyika katika mji wa Accra Ghana.
Taarifa za awali kuhusu kuagwa Mwili wa marehemu zinasema kwamba mwili Steven Kanumba unatarajiwa kuagwa siku ya Jumanne ya tarehe 10 Aprili, pale Leaders Club!

No comments: