P-FUNK IS MAKING A LOT OF SENSE!! PEOPLE IN THE SOCIAL NETWORKS ARE PROPAGATING WHAT P-FUNK HAS SAID!!

ALBERT MANGWEA: Mimi nilianza kumtambua kwa jina hilo aliponikuta Mazengo high school nikiwa kidato cha pili na YEYE cha kwanza.Kwa kuwa nilikuwa bwana mdogo sana basi hatukukawia kuwa na ukaribu pia ikichangiwa na hali ya wote kupenda kwenda Area "C" sehemu maarufu Dodoma kubadili chakula kwa weekend (si unajua mambo ya boarding school!!).Wakati nipo form four (Ngwair akiwa form 3) alipaa kwa umaarufu Dodoma kutokana na kipaji chake kikubwa cha kucheza basketball kiasi kwamba tulim'batiza jina la Mang' air (kutokana na uwezo wake wa kunata hewani akiwa anashoot tokea mbali).Ghafla akaanza kuipenda Rap na R&B na kuimudu huku akimwigilizia sana nguli Cisco wa mbele (wimbo alioupenda ni "How deep is your love").Hapo wote Mazengo tulimwita Sisqo.Mwaka 2006 nikakutana nae Dsm nikiwa na wanafunzi wenzangu wa chuo kikuu tukitafuta proffesional shooting digital camera iliyoibiwa na muhuni mmoja na Ngwair hakusita kutupa ushirikiano wake alituelekeza tukamuone M 2 P angetupeleka kwa mwizi wetu na kweli baadae tukaja kufanikiwa.Nikawa naendelea kuwasiliana nae hapa na pale na mara ya mwisho tukakutana Regence Park Hotel akiwa na jopo lake sote tukiangalia mechi za mwishoni za EPL na kutokana na msongamano wa watu sikufanikiwa kumkaribia na kumsalimia.Kwa mtu aliyepata kumjua Albert sharti afahamu kuwa jembe hakuwa mkorofi,hana visasi,mpole,nyenyekevu,hajivuni na ni nadra sana kuongea na hii haijachangiwa na ulevi wa aina yoyote bali ni tabia asilia za maisha yake.Mimi ni shabiki namba moja wa Ngwair tangu alipoanza muziki Room number 4 Ujamaa domitory pale ilipokuwa Mazengo High school.R.I.P Sisqo wa bongo Albert Mangwea.
Like ·  ·  · 22 minutes ago near Dar es Salaam ·

No comments: